PONGEZI KWA JESHI LA POLISI TANZANIA KATIKA KUSHEREHEKEA MIAKA 60 .
KWA HESHIMA NA TAADHIMA NAOMBA NISEMA KUWA, KATIKA KUMBUKUMBU ZANGU AMBAZO KWA BAHATI MBAYA ZINAENDELEA KUFIFIA, NI KWAMBA BABA WA TAIFA MWALIMU J K NYERERE AKISAIDIANA NA VIONGOZI WENZAKE, KADIRI SIKU ZILIVYOKWENDA, WAO BAADA YA UHURU DAIMA WALILENGA KUFANYA MABADILIKO/MABORESHO MAKUBWA NDANI YA JESHI LA POLISI * ILI KUIMARISHA TABIA ZA HAKI, USAWA WA BINADAMU ,NA UMOJA.
MAREKEBISHO MENGINE YALIKUWA NI KUONDOA HARAKA TABIA MBAYA ZA KIKOLONI AMBAZO ZILIKUWA ZA KIKATILI SANA KWA RAIA NA BADALA YAKE KULIANZISHWA MAFUNZO MAALUMU YALIYO HIMIZA USHIRIANO NA WANANCHI/RAIA WA TANZANIA.
MAONO YA WAASISI WA TAIFA HILI YALIHIMIZA *POLISI KUJIVUNA KUWA WAO NI WATUMISHI NA WALINZI WA USALAMA WA RAIA NA SIYO WAKANDAMIZAJI*
ENEO JINGINE KUBWA ZAIDI AMBALO DAIMA LILISISITIZWA NA MŴALIMU J K NYERERE LILIKUWA NI
* KUZINGATIA UADILIFU, UZALENDO, UTAIFA NA UWAJIKAJI IKIWA NI PAMOJA NA KUEPUKA TABIA YA KUTESA/KUNYANYASA WATUHUMIWA/ MAHABUSU*
KATIKA ENEO HILI WAASISI WA TAIFA HILI WALITOA ANGALIZO KUWA KUPIA TABIA HIZO ZA KUTESA WATUHUMIŴA
POLISI KWA BAHATI MBAYA SANA ,
**WALIKUWA WANARUTUBI
SHA AU WANAPOTEZA TAARIFA MUHIMU SANA ZA HIARI KUTOKA KWA WATUHUMIWA*
***WAASISI WA TAIFA LETU KWA IMANI KUBWA SANA WALISI
SITIZA JUU YA THAMANI KUBWA YA IMANI ISIYO NA HOFU KUWA NDIYO SILAHA YA THAMANI KUBWA ZAIDI KWA AFISA WA POLISI ANAYE ENDESHA UPELELEZI IWE NI AFISA WA POLISI AU USALAMA WA TAIFA . WAASISI WA TAIFA HILI BILA KUMUNG’UNYA MANENO WALIWEKA BAYANA KUWAMATESO KWA MTUHUMIWA NI KINYUME CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU NA KAMWE HAYATALETA MAJIBU SAHIHI KWA KAZI ILIYO KUSUDIWA !!!*
WALISISITIZA KUWA TABIA ZA AINA HIYO NI SERIKALI KUJITENGEZEA BOMU LA CHUKI KUBWA IKIWA NI PAMOJA NA KULIINGIZA TAIFA ***HASARA KUBWA YA KUPOTEZA TAARIFA MUHIMU KUTOKA KWA WATUHUMIWA PAMOJA NA WANAHABARI NA TAASISI NYINGINEZO KUTOKA NDANI YA JAMII.
RUSHWA NA UKATILI NDANI YA JESHI LA POLISI KUNA WAKATI HAYO NA MENGINEYO YALIIBUKA KUWA NI MATATIZO MAKUBWA SANA. KUFUATIA KADHIA HIYO NAKUMBUKA MWALIMU J K NYERERE MARA MBILI ALILAZIMIKA KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA SANA KATIKA UONGOZI WA JUU KWA KUTENGUA BAADHI YA VIONGOZI WAKUU NA KULISUKA UPYA JESHI LA POLISI ( BAHATI MBAYA NIMESAHAU MIAKA ,KATIKA HILO NAOMBA MSAADA KUJUA TAREHE MIEZI NA MIAKA).
NI KATIKA MATUKIO HAYO NDIPO MWALIMU J K NYERERE ALIPO HIMIZA JUU YA *KUUNDA/KUBORESHA JESHI LA POLISI LENYE UWAZI, UWAJIBIKAJI NA MAFUNZO YENYE UTAALAMU MKUBWA , IKIWA NI PAMOJA NA KUONDOA ATHARI ZA UKOLONI BAADHI ZIKIWA NI PAMOJA NA UKANDAMIZAJI WA HAKI ZA MSINGI ZA RAIA*
KATIKA ENEO HILI MWALIMU J K NYERERE ALIHIMIZA JUU YA MAFUNZO YENYE UBORA MKUBWA NA HAPO NDIPO ALIPO SISITIZA KUWA LAZIMA BAADHI YA VIJANA WENGINE WAPELEKWE KATIKA MATAIFA RAFIKI ILI WAPATE ELIMU BORA YA KISASA YENYE KUAKISI KAULI YA **ULINZI WA RAIA , HAKI NA MALI ZAO NA BAADAYE ILIIBULIWA SERA YA ULINZI SHIRIKISHI YAANI
* *POLISI JAMII*.
NYONGEZA YA MAFUNZO YALIYO SISITIZWA NI JUU YA POLISI KUHESHIMU HAKI ZA BINADAMU NDANI YA JAMII KWA MASILAHI YA MAENDELEO YA WATANZANIA.
SUALA JINGINE MUHIMU LILILO TILIWA MKAZO NI *POLISI KUKIRI KUWA MUDA WOWOTE MAHALI POPOTE WAO NI WAHUDUMU WAAMINIFU NA WENYE UTAYARI WA KUWAHUDUMIA WANANCHI WA TANZANIA KWA WAKATI MWINGINE KUJITOA SADAKA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU*
SIKU HIZI TUNAPO SONGA MBELE KATIKA UJENZI WA TAIFA LETU LA TANZANIA
KWA HESHIMA NA TAADHIMA NAOMBA KILA ALIYEMO NDANI YA JESHI LETU ZURI LA POLISI TANZANIA ***KWA KUPITA KIAPO CHAKE, DAIMA AJIULIZE KWA DHATI KUWA , JE ANAITENDEA HAKI JAMII YA WATANZANIA KATIKA USTAWI WA MAISHA YETU ?
TUTAFAKARI PAMOJA !
TAFADHALI NAWASILISHA KWENU HIZO PONGEZI ZANGU.
MZEE
KASORI SAMUEL H
SAA O7.41 USIKU KUAMKIA
JUMATANO
19/O9/2024