Habel Chidawali-Dodoma
WAKAZI zaidi ya 4,500 wa Mitaa ya Pinda na Majengo katika Kata ya Zuzu Jijini Dodoma wameikimbia adha ya ukosefu wa maji waliyokuwa nayo kwa kipindi kirefu baada ya kunufaika na mradi wa maji safi na salama.
Ukarabati wa kisima hicho ni sehemu ya miradi mikubwa iliyofadhiriwa na Japan ambayo hadi sasa imewekeza zaidi ya Dola 4.2 bilioni tangu ilipoanza kuisaidia Tanzania mara baada ya Uhuru.
Katika Mitaa ya Majengo na Pinda ndani ya Kata ya Zuzu kulikuwa na shida ya upatikanaji wa maji baada ya kisima kilichochimbwa mwaka 1991 kuharibika kulikopelekea wananchi kutumia zaidi ya saa mbili kutafuta maji ambayio hata hivyo hayakuwa salama.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Joshua Kajenge anasema hali ilikuwa mbaya kabla na kwmaba shughuli nyingi za kiuchumi zilikuwa zinasimama hasa nyakati za kiangazi kwani muda mwingi wa uzalishaji ulitumika kutafuta maji.
Kajembe anasema tangu mradi huo ulipokarabatiwa, wananchi upatikanaji wa maji umekuwa wa uhakika licha ya ukweli kuwa kuna miundombinu mingine ikiwemo tanki kubwa la kuhifadhi maji bado ni bovu.
“Kwanza tulikuwa na vituo sita tu vya kuchotea maji,lakini kwa sasa tumefikisha vituo karibu 12 na wateja wa majumbani wanaoweza kufikia 400 wamevuta maji, mifugo inakunywa lakini wengine wanamwagilia mboga zao,” anasema Kajembe.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini Wilaya ya Dodoma Mohamed Mbaga anasema mradi huo umekuwa na manufaa makubwa kwani umepunguza sehemu kubwa ya mahitaji ya maji yaliyokuwepo na kuwafanya wananchi kutumia muda mwingi kwenye shughuli za uzalishaji.
Mbaga anasema awali kulikuwa na kisima kilichochimbwa kwa mategemeo ya kuhudumia watu 200 lakini kwa sasa idadi imeongezeka na kukaribia watu 5000 hivyo mradi wa awali usingeweza kuwatosha.
“Licha ya ukweli kuwa maji hayatoshi kwa asilimia 100, lakini imesaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kuendelea kunufaika kwa karibu, bado tunasumbuliwa na tanki ambalo lina uwezo wa kuhifadhi maji kwa lita za ujazo 90,000 lakini kwa sasa tunahifadhi lita za ujazo 45,000 ambayo ni nusu,” anasema Mbaga.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake, Zainabu Ayubu ananaeleza kuwa ndoa nyingi kwenye mitaa hiyo zilikuwa na migogoro kutokana na watu kutokuaminiana kwa madai ya kuchelewa kwenye maji.
Zainabu anasema kazi yakufuata maji ilikuwa ni ngumu kwa mara ningi iliwabidi kudakma mapema alfajiri na hivyo kufanaya ndoa nyingi kuwa kwenye mashaka lakini wa ukarabati za kisima ulivyoingia wakajua wamepata ukombozi.
$$$$$$$$$$