Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dk Pindi Chana
WAZIRI CHANA AZINDUA ZAHANATI YA IVILIKINGE-MAKETE
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana amezindua zahanati ya Ivilikinge iliyopo Wilayani Makete Mkoani Njombe sambamba na kukabidhi vifaa mbalimbali vya hospitali vilivyotolewa na Benki ya NMB.
Katika hafla ya huo, Dk Chana amesema uwepo wa zahanati hiyo ni miongoni mwa vipaumbele vya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan vya huduma za afya zinawafikia wananchi mpaka vijijini.
” Hizi ni baadhi ya huduma tulizoahidi kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi hivyo tunapochagua viongozi tuchague ambao watatuletea maendeleo” amesisitiza Balozi Dk. Chana.
Waziri huyo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Njombe amesema kuwa kupitia zahanati hiyo wananchi wa Isapulano na vijiji vya jirani watapata huduma bora za afya na kuwaomba wananchi hao heshima wanaitumia ipasavyo zahanati hiyo.
Naye, Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Willy Mponzi amesema kwa juhudi za Rais kutoa huduma bora za afya vijijini na vijijini, changamoto za Sekta ya Afya ni kipaumbele kwa Benki ya NMB kwa afya na ushauri. kwa maendeleo ya Taifa lolote.
Benki ya NMB ina vifaa mbalimbali vya hospitali kwa zahanati hiyo ikijumuisha Vitanda vya kujifungulia (2),Vitanda vya uchunguzi (2),vitanda vya hospitali (5),Magodoro (5),folding screen (4),folding stretcher (2), delivery kit (5),drip stend(5), mashuka 50 na viti vya magurudumu (3) thamani ya zaidi ya shilingi milioni9.
Awali, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Mganga Mkuu wa Zahanati ya Isapulano, Hassan Omar alisema kuwa mradi huo umegharimu takribani milioni 146.1 ambayo inatokana na mchango wa wananchi (milioni 26.5), Wadau wazawa (milioni 6.6, Mbunge wa Jimbo la Makete, Mhe. Festo Sanga (milioni 4) ,Diwani (laki 5 na elfu 30), Benki ya NMB Mabati (milioni 8.5) na Serikali (milioni 100).
Amefafanua kuwa lengo la mradi huo ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Ivilikinge na vijiji jirani, umbali wa kufikia huduma kwa mama wajawazito, watoto na wazee.