Mwandishi Wetu -Dar
HATIMAE Treni ya abiria iliyotarajia kuanza safari saa 12:55 jioni kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, imeshaanza safari baada ya kuchelewa kwa takriban dakika 400.
Safari ya kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma imeanza saa 7: 32 usiku
Abiria wanaosafiri kwa Treni hiyo ya mwendo. kasi walifika Kituo cha TRC Dar es Salaam saa 10 ikiwa ni saa mbili kabla ya kuanza safari kama inavyoelekeza kwenye tiketi zao.
Hata hivyo, mchache kabla ya muda wa kuanza safari, yalianza kutolewa matangazo kuwa chombo hicho cha usafiri kingeondoka saa 4:20 usiku.
Kipindi chote cha matangazo ya kunadiri muda wa safari hakuna sababu ya kujua kuchelewa kwa Treni zaidi ya kusema sababu zilizo nje ya uwezo wao.
Hali iliendelea hivyo jambo lililozusha hasira za abiria hata wakaamza kupiga wakilalamika njaa kwao na watoto wao.
Sauti za abiria katika Kituo hicho ni kama zilisikika kwa viongozi wa juu na majira ya saa tano kuingia kikosi cha wahudumu wakaanza kugawa maji, soda na vitafunwa Kwa kila mmoja.
&&&&__&&&&