Mwandishi Wetu, Dodoma
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli zitakazotumika kuanzia Jumatano ya
ya leo Februari 5, 2025 saa 6:01 usiku.
Kwa mwezi Februari 2025, bei za rejareja na za jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara itakuwa kama zinavyoonekana katika Jedwali Na. 1 na 2, mtawalia.
Bei Kikomo za Rejareja (Shilingi/Lita)
Bandari Petroli Dizeli Mafuta ya Taa
Dar es Salaam petrol 2,820 dizeli 2,703 na Mafuta ya taa 2,710
Tanga petroli 2,825 dizeli 2,749 na mafuta ya taa 2,756
Mtwara petrol 2,892 dizel 2,775 mafuta ya taa 2,782
Jedwali 2: Bei Kikomo za Jumla (Shilingi/Lita)
Bei za mafuta za rejareja kwa maeneo mbalimbali ya miji, wilaya na mikoa kama ilivyoelekezwa na Mkurugenzi wa EWURA Dk James Mwainyekule ni kama
zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 3.
Bidhaa za mafuta zinazoagizwa na kupokelewa nchini zinazingatia bei za mafuta
yaliyosafishwa (FOB) kutoka soko la Uarabuni ambapo Februari 2025, bei kikomo za mafuta zimekokotolewa kwa kuzingatia bei za mwezi Januari 2025. Ikilinganishwa na mwezi Desemba 2024.
Kwa mujibu wa EWURA, bei za mwezi Januari zimeongezeka kwa asilimia 3.82 kwa mafuta ya petroli; asilimia 6.77 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 5.87 kwa mafuta ya taa.
Gharama za uagizaji mafuta (Premiums) zimepungua kwa wastani wa asilimia 4.90 kwa petroli, asilimia 14.94 kwa dizeli na wastani wa asilimia 0.81 kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Dar es Salaam huku kukiwa hakuna mabadiliko katika Bandari ya Tanga na zimepungua kwa wastani wa asilimia 6.34 kwa mafuta ya petroli na dizeli katika Bandari ya Mtwara.
Gharama za mafuta (FOB) na gharama za uagizaji (Premiums) zinalipiwa kwa kutumia fedha za kigeni ikiwemo Dola ya Marekani na kwa gharama za kubadilisha fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) umeongezeka kwa asilimia 4.77.
“Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 3 huku wafanyabiashara wa bidhaa za
mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2,” inasema sehemu ya Taarifa.
Kwa mujibu wa EWURA, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka agizo hili.
Msisitizo umewekwa kwa kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja pamoja na jamii kuzingatia bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo ambapo huduma hiyo inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi.
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei
za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA
itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa
za mafuta.
Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya
ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap) au kuwa chini
ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa
Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022
zilizotangazwa tarehe Januari 28, 2022 kupitia Gazeti la Serikali Na. 57 na
marekebisho ya Kanuni tajwa kupitia Gazeti la Serikali Na. 761A Oktoba 30,2023 na Mabadiliko ya Kanuni za Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja za Mwaka 2024.
JEDWALI NA. 3: Bei Kikomo za Rejareja – TZS/Lita Na Mji
Bei Kikomo
Petroli Dizeli Mafuta Ya Taa
1 Dar es Salaam 2,820 2,703 2,710
2 Arusha 2,882 2,787 2,794
3 Arumeru (Usa River) 2,882 2,787 2,794
4 Karatu 2,900 2,805 2,813
5 Longido 2,893 2,798 2,805
6 Monduli 2,887 2,792 2,800
7 Monduli-Makuyuni 2,892 2,797 2,805
8 Ngorongoro (Loliondo) 2,967 2,879 2,886
9 Pwani (Kibaha) 2,825 2,707 2,715
10 Bagamoyo 2,831 2,714 2,721
11 Bagamoyo (Miono) 2,862 2,745 2,752
12 Bagamoyo (Mbwewe) 2,843 2,726 2,733
13 Chalinze Junction 2,834 2,717 2,724
14 Chalinze Township (Msata) 2,839 2,721 2,729
15 Kibiti 2,841 2,723 2,731
16 Kisarawe 2,827 2,710 2,717
17 Mkuranga 2,830 2,713 2,720
18 Rufiji 2,848 2,731 2,738
19 Dodoma 2,879 2,762 2,769
20 Bahi 2,886 2,769 2,776
21 Chamwino 2,874 2,757 2,764
22 Chamwino (Mlowa) 2,886 2,769 2,776
23 Chemba 2,906 2,788 2,795
24 Kondoa 2,912 2,795 2,802
25 Kongwa 2,876 2,759 2,766
26 Mpwapwa 2,880 2,763 2,770
27 Mpwapwa (Chipogoro) 2,892 2,775 2,782
28 Mtera (Makatopora) 2,898 2,781 2,788
29 Mvumi 2,886 2,768 2,775
30 Geita 2,986 2,868 2,876
31 Bukombe 2,975 2,857 2,865
32 Chato 3,007 2,889 2,897
33 Mbogwe 3,024 2,906 2,914
34 Nyang’hwale 3,001 2,883 2,891
35 Iringa 2,884 2,767 2,774
36 Ismani 2,890 2,772 2,780
37 Kilolo 2,889 2,771 2,779
38 Mufindi (Mafinga) 2,894 2,777 2,784
39 Mufindi (Igowole) 2,903 2,786 2,793
40 Mufindi (Mgololo) 2,906 2,789 2,796
41 Kagera (Bukoba) 3,036 2,918 2,926
42 Biharamulo 3,010 2,893 2,900
43 Karagwe (Kayanga) 3,052 2,935 2,942
44 Kyerwa (Ruberwa) 3,058 2,941 2,948
45 Muleba 3,036 2,918 2,926
46 Ngara 3,024 2,906 2,914
47 Misenyi 3,044 2,927 2,934
48 Katavi (Mpanda) 2,978 2,861 2,868
49 Mlele (Inyonga) 2,960 2,842 2,850
50 Mpimbwe (Majimoto) 2,997 2,880 2,887
51 Tanganyika (Ikola) 2,996 2,879 2,886
Mji
Bei Kikomo
Petroli Dizeli Mafuta Ya Taa
52 Kigoma 2,983 2,865 2,873
53 Uvinza (Lugufu) 2,973 2,856 2,863
54 Muyobozi Village (Uvinza) 2,985 2,867 2,875
55 Ilagala Village (Uvinza) 2,987 2,870 2,877
56 Buhigwe 2,981 2,864 2,871
57 Kakonko 2,983 2,866 2,873
58 Kasulu 2,992 2,874 2,882
59 Kibondo 2,989 2,872 2,879
60 Kilimanjaro (Moshi) 2,872 2,777 2,784
61 Hai (Bomang’ombe) 2,875 2,780 2,787
62 Mwanga 2,865 2,770 2,777
63 Rombo (Mkuu) 2,888 2,798 2,805
64 Same 2,858 2,763 2,770
65 Siha (Sanya Juu) 2,878 2,783 2,790
66 Lindi 2,879 2,762 2,769
67 Lindi-Mtama 2,897 2,780 2,787
68 Kilwa Masoko 2,854 2,737 2,744
69 Liwale 2,900 2,783 2,790
70 Nachingwea 2,908 2,791 2,798
71 Ruangwa 2,910 2,793 2,800
72 Manyara (Babati) 2,916 2,825 2,833
73 Hanang (Katesh) 2,927 2,836 2,843
74 Kiteto (Kibaya) 2,931 2,836 2,844
75 Mbulu 2,929 2,838 2,845
76 Simanjiro (Orkasumet) 2,948 2,857 2,865
77 Mara (Musoma) 2,986 2,869 2,876
78 Musoma Vijijini (Busekela) 2,999 2,881 2,889
79 Rorya (Ingirijuu) 2,993 2,876 2,883
80 Rorya (Shirati) 3,001 2,884 2,891
81 Bunda 2,977 2,860 2,867
82 Bunda (Kisorya) 2,990 2,872 2,880
83 Butiama 2,983 2,866 2,873
84 Serengeti (Mugumu) 2,994 2,877 2,884
85 Tarime 2,995 2,877 2,885
86 Tarime (Kewanja/Nyamongo) 3,000 2,883 2,890
87 Mbeya 2,927 2,810 2,817
88 Chunya 2,937 2,820 2,827
89 Chunya (Makongolosi) 2,942 2,825 2,832
90 Chunya (Lupa Tingatinga) 2,944 2,827 2,834
91 Kyela 2,943 2,826 2,833
92 Mbarali (Rujewa) 2,911 2,794 2,801
93 Rujewa (Madibira) 2,925 2,807 2,815
94 Rujewa (Kapunga) 2,921 2,804 2,811
95 Rungwe (Tukuyu) 2,936 2,819 2,826
96 Busokelo (lwangwa) 2,945 2,828 2,835
97 Morogoro 2,845 2,728 2,735
98 Mikumi 2,861 2,744 2,751
99 Kilombero (Ifakara) 2,883 2,766 2,773
100 Kilombero (Mlimba) 2,906 2,788 2,795
101 Kilombero (Mngeta) 2,895 2,777 2,785
102 Ulanga (Mahenge) 2,894 2,776 2,784
103 Malinyi 2,904 2,787 2,794
104 Kilosa 2,864 2,746 2,754
105 Gairo 2,864 2,746 2,754
106 Mvomero (Wami Sokoine) 2,856 2,738 2,746
107 Mvomero (Sanga Sanga) 2,845 2,728 2,735
108 Turian 2,870 2,753 2,760
109 Mtwara 2,893 2,775 2,783
110 Nanyumbu (Mangaka) 2,942 2,824 2,832
111 Masasi 2,918 2,801 2,808
112 Newala 2,925 2,807 2,815
113 Tandahimba 2,918 2,801 2,808
114 Nanyamba 2,918 2,801 2,808
115 Mwanza 2,970 2,853 2,860
116 Kwimba 2,988 2,871 2,878
117 Magu 2,979 2,861 2,868
118 Misungwi 2,965 2,847 2,855
119 Misungwi (Mbarika) 2,975 2,858 2,865
120 Sengerema 3,003 2,886 2,893
121 Ukerewe 3,030 2,913 2,920
122 Njombe 2,913 2,795 2,803
123 Luponde 2,919 2,802 2,809
124 Njombe (Kidegembye) 2,933 2,816 2,823
125 Ludewa 2,951 2,833 2,841
126 Makambako 2,905 2,788 2,795
127 Makete 2,944 2,826 2,834
128 Wanging’ombe (Igwachanya) 2,910 2,793 2,800
129 Rukwa (Sumbawanga) 2,993 2,876 2,883
130 Sumbawanga Rural (Mtowisa) 2,993 2,876 2,883
131 Kalambo (Matai) 3,000 2,883 2,890
132 Nkasi (Namanyele) 3,007 2,889 2,897
133 Kabwe 3,021 2,904 2,911
134 Nkasi (Kirando) 3,016 2,899 2,906
135 Ruvuma (Songea) 2,944 2,826 2,834
136 Mbinga 2,956 2,839 2,846
137 Namtumbo 2,949 2,832 2,839
138 Nyasa (Mbamba Bay) 2,967 2,849 2,856
139 Tunduru 2,923 2,806 2,813
140 Kizuka 2,955 2,837 2,845
141 Shinyanga 2,949 2,832 2,839
142 Kahama 2,954 2,836 2,844
143 Kishapu 2,957 2,840 2,847
144 Ushetu (Nyamilangano) 2,966 2,848 2,855
145 Ushetu (Kangeme Village) 2,971 2,854 2,861
146 Salawe 2,963 2,846 2,853
147 Simiyu (Bariadi) 2,967 2,850 2,857
148 Busega (Nyashimo) 2,979 2,862 2,869
149 Itilima (Lagangabilili) 2,967 2,850 2,857
150 Maswa 2,961 2,844 2,851
151 Meatu (Mwanhuzi) 2,972 2,855 2,862
152 Singida 2,911 2,794 2,801
153 Iramba 2,923 2,806 2,813
154 Manyoni 2,896 2,778 2,786
155 Itigi (Mitundu) 2,911 2,794 2,801
156 Ikungi 2,906 2,789 2,796
157 Misigiri 2,923 2,806 2,813
158 Mkalama (Nduguti) 2,936 2,818 2,826
159 Songwe (Vwawa) 2,937 2,819 2,827
160 Songwe (Mkwajuni) 2,944 2,826 2,834
161 Ileje 2,941 2,823 2,831
162 Momba (Chitete) 2,946 2,828 2,836
163 Tunduma 2,941 2,823 2,831
164 Tabora 2,929 2,811 2,818
165 Igunga 2,928 2,811 2,818
166 Kaliua 2,942 2,824 2,831
167 Ulyankulu 2,939 2,822 2,829
168 Nzega 2,939 2,822 2,829
169 Sikonge 2,937 2,820 2,827
170 Urambo 2,938 2,821 2,828
171 Uyui 2,935 2,817 2,825
172 Mpyagula 2,960 2,843 2,850
173 Tanga 2,825 2,749 2,756
174 Handeni 2,846 2,728 2,736
175 Kilindi 2,861 2,763 2,770
176 Korogwe 2,838 2,742 2,749
177 Lushoto 2,847 2,752 2,759
178 Lukozi 2,853 2,757 2,764
179 Bumbuli 2,856 2,760 2,768
180 Mkinga (Maramba) 2,832 2,763 2,771
181 Muheza 2,830 2,749 2,756
182 Pangani 2,833 2,756 2,763