Mwandishi Wetu-Kibaha
WAHITIMUwa Mafunzo ya Ufundi (VETA) Mkoa wa Pwani wameiomb Serikali kuweka utaratibu wa kuwapa mikopo ili nao waweze kujikimu wakiwa kwenye Mafunzo kwa vitendo kwani unaweza kukutana na changamoto na kufanya kujifunza kwao kuwa mgumu.
Wamesema hayo wakati wa sherehe ya mahafali ya 14 ya Chuo Cha VETA yaliyofanyika Kibaha ambapo jumla ya wanafumzi 102 walihitimu Mafunzo yao baada ya kuwa masomoni hapo kwa miaka miwili.
Wahitimu hao wamesema changamoto wanayokumbana nayo ni pale wanapokwenda kufanya Mafunzo kwa vitendo wanatakiwa kujigharamia na wakati huo wanakuwa hawana ajira hivyo kujikuta kwenye wakati mgumu na baadhi yao kukatisha muda waliotakiwa kufanya vitendo.
“Tunapangiwa kufanya kazi kwa vitendo katika maeneo mbalimbali ya viwandani na tukiwa huko tu fedha za matumizi ili kukidhi mahitaji yetu lakini wakati huo bado tu ya ajira hivyo tunaishi kwa ugumu,”amesema Suzana Kinyunyu wakati akisoma risala.
Kinyunyu kuongeza kuwa iwapo Serikali italifanyia kazi ombi lao, watakuwa na uwezekano wa kujifunza kwa vitendo na kujiongezea ujuzi kabla ya kuajiriwa ama kujiajiri kwani watakuwa na ujuzi wa kiwango Cha juu.
Awali Mkuu wa Chuo hicho Clara Kibodya alisema ingawa wanaendelea kupata mafanikio kwa kuwapa vijana ujuzi, lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kutoka kwa mabweni na kukosea unaozunguka Chuo hicho kwa ajili ya usalama wa vijana wao.
“Tunahitaji kuwa na mabweni mawili kwa ajili ya wasichana yaliyopo hivi sasa hayatoshelezi kulingana na idadi tuliyonayo hivyo tunawaomba wadau wajitokeze kutuunga mkono,” amesema Kibodya.
Kuhusu uzio Mkuu huyo amesema kuwa ukijengwa uimarisha ulinzi wa Chuo na Mali lakini usalama utaimarika huku tukikipa Chuo.
Akijibu risala hiyo mgeni rasmi kwenye mahafali hayo Asma Mwinyi aliahidi kutoa mifuko 100 ya saruji ili kuunga mkono katika changamoto hiyo huku akionba wadau wengine kujitokeza kuwashika mkono VETA Pwani.
Asma amesema kwa namna yoyote Chuo hicho kinahitaji mabweni mazuri, madarasa pamoja na maeneo rafiki ya kujifunzia hivyo Kuna ya kufanya kila namna ili kuboresha Chuo hicho ambacho ni tegemeo la kuboresha watu wenye ujuzi.
Katika hatua nyingine Asma amewataka wahitimu hao kuzingatia maadili mema kokote watakakokwenda na kuwa mabalozi wazuri kwa yale waliyojofunza miaka miwili kwani tayari wamejiweka kwenye uthamani na usalama wa maisha yao.
Mwisho,…