Habel Chidawali,Dodoma
USIKU wa kuamkia Desemba 21,2024 umekuwa wa majonzi kwa wakazi wa Nzuguni kufuatia kifo cha mtoto Emmanuel Elias aliyekuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu baada ya kutumbukia kwenye shimo la choo huku mazingira ya kifo chake yakiacha utata.
Umati wa watu wakiwemo viongozi na vyombo vya ulinzi na usalama walikusanyika katika la nyumba ya Sofia Njiba ambayo inaishi wapangaji.
Mwili wa mtoto huyo umeopolewa na kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji majia ya saa tano usiku lakini wananchi wameho juu ya mazingi ya kifo ha mtoto huyo malaik.
Akizungumza mara baada ya kuutoa shimoni mwili huo, Afisa Oparesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Dodoma Ispekta Deogratius Inano amesema kifo cha mtoto huyo kinazua maswali mengi lakini jambo la msingi ni wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao hasa kipindi hiki ambacho shule zimefungwa.
Kwa mujibu wa Inspekta Inano, mkoa wa Dodoma na hasa Kata ya Nzuguni kumekuwa na matukio ya watoto kutumbukia kwenye mashimo mara nyingi hasa nyakati za msimu wa mvua huku sababu zikitajwa kuwa ni mashimo yanayoachwa wazi bila kufunikwa.
“Kwa Nzuguni hili ni tukio la kwanza, lakini ni tukio la pili ndani ya kipindi hiki kwani juzi tumeopoa mwili wa mtoto wa miaka 10 katika Kata ya Mkonze aliyekufa kwa kutumbukia kwenye dimbwi, wazazi na walezi tuwe makini na watoto wetu nyakati hizi,” amesema Inano.
Kwa mujibu maelezo ya Inano,inashangaza kwani mama wa mtoto wai akimtafuta mwanawe, kuna mtu alikwenda kuweka karatasi mlangoni iliyoandikwa ‘mtoto wako ametumbukia kwenye shimo, sitaki ushahidi’ kitendo kinachoonyesha kuna mtu alishuhudia tukio hilo lakini hakusema hadi saa 4 zilipopita.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nzuguni Aloyce Luhega alipiga marufuku kuwepo kwa mashimo ya wazi katika mitaa inayozunguka Kata hyo na kagiza viongozi wasimamie jambo hilo na yeyote atakayekaidi achukuliwe hatua.
Kingine amsisitiza ka wakazi wa mtaa huo kutokuchochea mgogoro ambao unaweza kusababisha uvunjifu wa amani badala yake watoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kama kuna mtu anayejua ukweli kuhusu kutumbukia kwa mtoto huyo na hasa mazingira yalivyokuwa.
Amesema mtindo wa kutofunika mashimo ya vyoo umekuwa kama mazoea kwa baadhi ya wananchi bila kujali mazingira halisi wanayoishi kwamba yanahatarisha usalama wao ikiwemo watoto wadogo ambao kipindi hiki cha likizo inakuwa ni kazi kuwalinda.
@@@@@@@@@@@@