VIONGOZI na Wakazi wa Mtaa wa Tangini Katika Halmashauri ya Kibaha Mkoani Pwani leo wameingia mtaani nyumba kwa nyumba kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye uandikishaji daftari la mkaazi ilikuwa na sifa ya kupiga kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Uandikishaji wa daftari hilo unataraji kuanza Oktoba 11 hadi 20,2024 nchini kote na Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuzindua mpango huo katika Kijiji cha Chamwino Mkoani Dodoma ambako atajiandikisha na ndiko atakakopigia kura Novemba 27,2024.
“Tunaamini watu wengi watajitokeza katika kipindi hiki kuanzia siku ya kwanza hadi mwisho na hata katika kipindi cha uchaguzi tunajua hali itakuwa nzuri katika mtaa wetu kwani viongozi wametoa hamasa ya kutosha na watu wamehamasika zaidi,”amesema Idd Mfaume.
Mchakato wa ndani kwa vyama vya siasa katika kuwatafuta wagombea umeshaanza ambapo Chama Cha Mapinduzi kimetoa ratiba kwa wanachama wake kuwa zoezi la kutoa fomu za kugombea litaanza Oktoba 20,2024 huku vyama vingine vikifanya maandalizi ya wagombea wake.
Juzi Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika alitangaza kuwa Mtanzania yeyote ambaye ni mwanachama wa chama hicho na asiye mwanachama lakini ana mapenzi na Chadema anaruhusiwa kugombea hivyo wenye nia wawasiliane na viongozi wa chama kwa ajili ya kuthibitishwa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu William Lukuvi juzi aliwatembelea viongozi wa vyama vya siasa na kuwapa tumaini la Serikali kuwa uchaguzi utakuwa Huru na Haki kama ambavyo kiongozi mkuu wa nchi amekuwa akitangaza wakati wote.
Uchaguzi huu unatarajia kuwa kipimo cha demokrasia katika Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa kwanza mwanamke Afrika Mashariki Samia Suluhu Hassan baada ya uchaguzi wa mwisho uliofanyika 2019 ambao ulilalamikiwa na wanasiasa pande zote nchini.
@@@@@@@@@@@@@