EWURA MWENYEJI MKUTANO WA MAMLAKA ZA UDHIBITI KUSINI MWA AFRIKA
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imekuwa mwenyeji wa vikao vya Kamati ndogo za Umoja wa Mamlaka za Udhibiti wa Sekta ya Nishati Kusini mwa Afrika (RERA) vilivyoanza rasmi Septemba 23,2024 Visiwani Zanzibar.
Miongoni mwa Mamlaka zinazoshiriki vikao hivyo ni kutoka Angola, Botswana, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho, Eswatini, Zambia, Malawi, Msumbiji, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania.
Kwa upande wa Zanzibar, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) imeshiriki kama mtazamaji kwa kuwa bado haijawa mwanachama wa umoja huo licha ya kuwa vikao vinafanyikiwa huko lakini EWURA ambaye ni mwanachama ndiye aliyepewa jukumu la weyeji.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa, vikao hivyo vitakafanyika kwa awamu mbili, kati ya Septemba 23-27 Oktoba 8-11,2024 huku vikitaraji kujadiri pamoja na mambo mengine, namna ya kuboresha shughuli za udhibiti wa nishati katika maeneo ya fedha, rasilimali watu, huduma kwa wateja, habari, mawasiliano na teknolojia ya habari.
Masuala mengine ni kuhusu udhibiti wa kiufundi na kiuchumi ikijumuisha bei, tozo na viwango vya huduma kwenye sekta za umeme.
$$$$$$$$$