Habel Chidawali-Dodoma
TAASISI ya Just Diggit imezindua mfumo wa Kijani App ambao unawawezesha wakulima kutunza mazingira kupitia mifumo ya kidigitali ambao unaweza kutunza mazingira.
Uzinduzi huo umefanyika leo Agosti 7,2024 na Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde ambaye ameomba Watanzania kujiunga katika mfumo huo ili kuwawezesha kutunza ardhi kwa faida ya kilimo na uzalishaji mazao.
Naibu Waziri amesema mfumo huo unawezesha wakulima kukutana moja kwa moja na wataalamu wa masuala ya kilimo ambao watakuwa tayari wakati wowote kuwapa elimu kuhusiana na masuala mazima ya kilimo na watakuwa na nafasi ya kuuliza maswali ya kitaalamu.
“Niwapongeze sana wenzetu hawa wa Just Diggit kwa hiki ambacho wamekifanya kwani ni kitu chema ambacho kitatusaidia sisi Serikali katika kuwafikia wakulima wetu na wananchi kwa ujumla, tunaunga mkono jambo hili kwa kutusaidia na kutunza mazingira,” amesema Silinde.
Akizungumzia mfumo huo, Meneja Ukijanishaji Ardhi wa Just Diggit Mary Sengelela, amesema mfumo wa Kijani App unapatikani kwenye simu zote za Android na kwamba hata ambao hawana simu janja wamekuwa na nafasi nzuri ya kupata ujumbe kupitia simu ndogo (viswaswadu).
Kwa Mujibu wa Meneja huyo, wamefanya kazi hiyo kwa kushirikiana na
Mary amesema mfumo huo una mambo Matano ambayo ni ukusara wa mwanzo, ukurasa wa maarifa uliosheheni kozi zote kwa ajili ya mkulima kufuata mbinu bora za kilimo, kuna ukurasa wa kikabu ambao unamsaidia mkulima kuchagua.
Kurasa zingine ni wasifu wa mtumiaji na kwamba inawarahishia watumiaji kwani ipo kwa njia ya video na sauti ambayo inawezesha watumiaji kupata uelewa mkubwa bila kuwa na kigugumizi cha namna yoyote.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&