Habel Chidawali- Dodoma
KATIBU Mkuu Kiongozi Dk Moses Kusiluka amepongeza mpango wa benki ya NMB katika kuwatumia wataalam wa kuwapa ushauri na maelekezo vijana wanaotaka kujiunga na shughuli za kilimo ili walime kwa tija.
Dk Kusiluka ametoa pongezi hizo alipotembelea maonyesho ya wakulima katika viwanja vya Nzuguni baada ya kuhoji kama benki hiyo itakuwa na wataalamu wa kutoa ushauri kwenye masuala ya kilimo hususani kundi la vijana.
Akiwa katika banda la benki ya NMB, Katibu Mkuu Kiongozi ametaka kujua ushiriki wa benki hiyo kwenye maonyesho katika kuwasaidia wakulima wa Tanzania ili wafikie malengo yao na kuongeza uzalishaji kwa ujumla na hasa kundi la vijana.
“Hayo yote ni sawa, lakini kwenye mipango hii ya utoaji wa elimu kwa vijana mnao wataalamu ambao mnawatumia kwa ajili ya kutoa elimu hiyo au mnatumia mbinu gani kufikisha ujumbe huo,”ameuliza Dk Kusiluka.
Akitoa maelezo mbele ya kiongozi huo, Meneja Mahusiano wa Mikopo Kanda ya Kati Mtolela Stephen amesema ndani ya benki hiyo kuna wataalamu maalumu kwa ajili ya kutoa elimu hiyo na mara nyingi wamekuwa wakifanya hivyo katika maeneo tofautitofauti.
Mtolela amesema ushiriki wao kwenye maonyesho ya wakulima unatokana na mahusiano waliyonayo kwenye sketa ya kilimo ikiwemo kutoa mikopo ya mbolea, madawa na kuwapatia mikopo mikubwa ya kununua zana za kilimo ikiwemo matrekta.
Kwa mujibu wa Meneja Mtolela, mikopo mingine wanayoitoa ni kwa ajili ya unenepeshaji wa mifugo ikiwemo ng’ombe ambako wafugaji wengi wamenufaika n ahata wakaongeza tija kwa wafugaji kupitia dirisha hilo.
Akizungumzia dhamana za mikopo hiyo amesema inatolewa kwa mtu mwenye nyumba hata kama haina hati ya umiliki ilimradi ikithibitika kuwa ni nyumba ya mhusika NMB inampa mkopo kwa ajili ya kutimiza malengo yake lakini wengine wanaweka dhamana za vifaa na mashamba.
&&&&&&&&&&&&&&&&