Kampuni ya Trouw Nutrition imekuja na suluhisho la matatizo ya muda mrefu waliyokuwa wakiyapata wafugaji ikiwemo kukosekana kwa ubora wa vyakula vya mifugo.
Meneja wa Trouw Nutrition Joseph Joachim amesema kila kitu kwao ni ukombozi kwa wafugaji kwani wamejipanga kwa ajili ya kuwahudumia wafugaji ikiwemo kutoa ushauri mzuri wa jinsi ya kulisha mifugo.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda ya Kampuni hiyo viwanja vya maonyesho Nanenane Nzuguni, Meneja amesema wanazo mashine nzuri za kisasa zinazosaidia wafugaji kutengeneza vyakula na kupima ubora wa vyakula na maji.
“Tunazo mashine za kisasa zinazorahisisha upimaji wa ubora wa malighafi au chakula cha mifugo ikiwemo unyevu, protin na wanga ili kumsaidia mtengenezaji wa chakula cha mifugo kuwa na uhakika juu ya ubora au malighafi husika,” amesema Joseph.
Kwa mujibu wa Mtaalamu huyo, wafugaji kwa sasa hawahitaji kuwa na usumbufu wa kuwaza namna ya kufuga kitaalam kwani kila jambo linawezekana mahali walipo kwa gharama nafuu lakini Trouw Nutrition pia wanasaidia kutoa ushauri na wakati mwingine kupima baadhi ya vitu kwa ajili ya mifugo bure.